Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame M. Mbarawa amezindua rasmi safari
za treni katika eneo la Kilosa na Gulwe ambalo lilikuwa limeathirika kutokana
na mvua zilizosababisha uharibifu wa miunbombinu ya reli katika eneo hilo na
kusimama kwa safari kwa takribani mwezi mmoja. Waziri Mbarawa katika ziara hiyo
aliyoifanya jana Tareh 11 February, ambapo alifungua njia hiyo kwa kuendesha
treni ya mizigo yenye behewa 20 kama ishara ya kurudisha upya safari za treni
kutoka Dar es Salaam kuelekea Bara.
Aidha katika
ziara hiyo Waziri Mbarawa ameeleza kuwa kutokana na kusimama kwa safari za
treni za mizigo na abiria kwa kipindi cha mwezi mmoja TRL imepoteza takriban
Bilioni 4 na amewahakikishia watumiaji wa usafiri huo kuwa huduma zimerejea.
Mara baada ya
kukagua ukarabati wa reli unaofanyika katika eneo hilo, Waziri Prof. Mbarawa
aliwatoa hofu wafanyabiashara wanaotumia usafiri wa treni za reli ya kati kuwa
mizigo yao iko salama, na kuwa kampuni ya reli imejipanga kutoa huduma bora
zaidi, pia Waziri Mbarawa aliongeza kwa kusema kuwa kuanzia sasa hivi mvua
zinazokuja mwezi wa tatu na wa nne reli itakuwa salama, waendelee kutumia
huduma za usafiri wa treni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipanda kwenye injini ya treni kwa ajili
ya kuendesha kuashiria kuanza rasmi kwa safari treni kati ya Kilosa na Gulwe
|
“Tuna kampuni
ya reli ya kisasa na tumejipanga zaidi kutoa huduma kwao wao iliyotukuka, mizigo
yao iko salama”, “Changamoto zilizotokea zimetokea ila nataka kuwahakikishia
kwamba kuanzia sasa hivi mvua zinazokuja mwezi wa tatu na mwezi wa nne reli itakuwa
salama na waendelee kuiamini reli yetu” Alisema Mbarawa.
Pia Waziri
Mbarawa alitoa wito kwa vibarua wanaofanya kazi kwenye ukarabati wa njia hiyo
ya reli na kuwataka wawe waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila
siku wawapo kazini ili kuepuka udokozi unaoweza kuisababishia hasara serikali.
Mkurugenzi wa TRL
akizungumza na wananchi wa maeneo ya Kilosa mara baada ya ufunguzi wa safari za
treni kati ya Kilosa na Gulwe
|
Mkurugenzi wa TRL Ndg.
Masanja Kadogosa akishiriki kazi na baadhi ya vibarua wanaoshiriki
kwenyenukarabati wa reli kati ya Kilosa na Gulwe.
|
No comments:
Post a Comment