\Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji
wa Shirika la Reli Tanzania Ndg. Focus Sahani Makoye amefanya ziara kwenye eneo
la Kilosa kukagua maendeleo ya uimarishaji wa njia ya reli kati ya Kilosa na
Gulwe, sehemu ambayo iliathiriwa zaidi na mafuriko yaliyosababishwa na mvua mwishoni
mwa mwaka jana na kusababisha safari za treni kutoka Dar es Salaam kuelekea
Bara kusitishwa kwa muda kwa takribani miezi miwili.
Katika hatua nyingine Serikali
imesema ifikapo mwezi wa saba mwaka huu wananchi wote wanaoendesha shughuli za
kibinadamu ikiwemo kilimo kandokando ya reli waache mara moja pindi
watakapovuna mazao yao ili kulinda reli kutokana na ukweli kwamba shughuli za
kibinadamu zinazoendelea kandokando ya reli zimechangia kwa kiasi kikubwa
kutokea kwa mafuriko katika eneo hilo la Kilosa hadi Gulwe.
Tamko hilo limetolewa na
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Ndg. Atashasta
Nditiye ambaye pia amefanya ziara katika eneo hilo kwa nyakati tofauti kwa
lengo la kujionea maendeleo ya ukarabati wa tuta la reli ambalo liliathiriwa
Vibaya na Mafuriko mwishoni mwa mwaka jana.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Fokasi Sahani
amewapongeza wafanyakazi wa Shirika hilo pamoja na wahandisi waliofanikisha
kurejea kwa safari za Treni, huku akizungumzia zoezi la upandaji wa matete
kandokando ya tuta la reli ambayo yatasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo.
Moja kati ya makaravati mapya ambayo yamejengwa kwenye tuta la reli kati ya Kilosa na Gulwe ili kuruhusu maji kupita kwenye njia sahihi bila kuleta athari kwenye tuta la reli..
|
No comments:
Post a Comment