SHIRIKA
LA RELI TANZANIA-TRC
YAH: AJALI YA BASI LA ABIRIA KUGONGA TRENI YA MIZIGO
KATIKA ENEO LA GUNGU MKOANI KIGOMA
Uongozi
wa Shirika la Reli Tanzania-TRC unapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu ajali ya
basi la abiria kugonga treni ya mizigo na kusababisha vifo vya watu kumi, kati
yao wanawake watatu na wanaume saba na majeruhi thelathini na mbili.
Ajali
imetokea jana tarehe 6 Juni, 2018 majira ya saa 12:15 Asubuhi katika eneo la Gungu Mkoani Kigoma. Ajali hiyo imesabababishwa na
basi la kampuni ya Princess Hamida lenye namba za usajili T885DLD, aina ya TATA,
lililokuwa likiendeshwa na Fredy Kawasange
kutoka Kigoma kwenda Tabora. Basi hilo limegonga treni ya mizigo yenye injini
namba 88U15 iliyokuwa ikitoka
Kazuramimba kwenda Kigoma.
Chanzo
cha ajali kimetokana na uzembe wa dereva kutofuata sheria za barabarani. Dereva
huyo wa basi hakusimama mita 15 kabla ya kivuko chetu cha gari Moshi na hivyo kusababisha ajali
hiyo.
Miili
ya marehemu imehifadhiwa katika
Hospitali ya Mkoa, Kigoma - Maweni kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi, na majeruhi
wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo ya Maweni.
Shirika
la Reli Tanzania-TRC linawapa pole wanafamilia wote walioguswa na ajali hiyo na
kusababisha majeruhi na vifo vya ndugu, jamaa na marafiki. Shirika linazidi
kuwaombea wawe na moyo wa subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu.
Shirika linaungana na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awapumzishe Marehemu mahala
pema peponi na Majeruhi wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya
kila siku.
Imetolewa na;
Idara ya Uhusiano kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Reli Tanzania
Dar es Salaam.
07/06/2018.
Innalilah wainaylayh rajiun
ReplyDelete