Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) unawataarifu
abiria wote na wananchi kwa Ujumla kuwa kutokana na kuharibiwa kwa
miundombinu ya reli kati ya stesheni za Kilosa na Gulwe kurokana na
mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha maeneo hayo huduma za reli
kutoka Dar es Salaam zimesitishwa.
Hata hivyo Uongozi baada ya kutathmini hali ya
miundombinu ya maeneo mengine yalio salama imeamua kuhamishia huduma ya usafiri
wa treni kutokea Dodoma kuanzia siku ya Jumanne Januari 16, 2018.
Ratiba ya huduma ya muda kuanzia Dodoma ni kama
ifuatavyo..
Uongozi wa TRL
bado unaendelea kusimamia kazi ya ukarabati wa eneo lililo haribika kati ya
Kilosa na Gulwe. Aidha Kampuni inaomba radhi Kwa
usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi ambacho huduma ya usafiri wa
treni haitakuwepo mpaka hapo itakaporejeshwa tena, wananchi watafahamishwa
rasmi kupitia vyombo vya habari.
Sehemu ya Reli ikiwa imeharibiwa vibaya na mvua kubwa
iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha mafuriko kwenye njia ya reli.
|
No comments:
Post a Comment