MKURUGENZI WA SHIRIKA LA RELI TANZANIA AHUDHURIA MKUTANO WA MIPANGO YA RASILIMALI ZA EAC - TRC Blog

Home Top Ad

"TOGETHER WE MOVE"

Wednesday, February 21, 2018

MKURUGENZI WA SHIRIKA LA RELI TANZANIA AHUDHURIA MKUTANO WA MIPANGO YA RASILIMALI ZA EAC

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Ndugu Masanja Kadogosa amehudhuria Mkutano wa Mipango ya Rasilimali za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofunguliwa jana tarehe 21 February Kampala nchini Uganda kwenye Hotel ya Munyonyo Speke.
Kwenye picha ni, Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Ndg. Masanja K. Kadogosa(aliyeketi kushoto), mkurugenzi wa Shirika la Reli la Uganda (URC) Ndg. Charles A. Kateeba(aliyeketi kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Ndg. Deusdedith Kakoko (aliyeketi katikati).
Katika mkutano huo Ndg. Kadogosa amekutana na wadau mbalimbali akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Mhe. Charles Mwijage, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Ndg. Deusdedith Kakoko, Mkurugenzi wa Shirika la Reli la Uganda (URC) na waandishi wa habari kwa lengo la kuwajulisha wafanyabiashara wa nchini Uganda kuhusu kuanza kutumika kwa njia ya Portbell hadi Kampala kutpitia reli ya kati (Central Line).
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Ndg. Masanja K. Kadogosa(aliyeketi kushoto), mkurugenzi wa Shirika la Reli la Uganda (URC) Ndg. Charles A. Kateeba(aliyeketi kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Ndg. Deusdedith Kakoko (aliyeketi katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Ndg. Masanja Kadogosa, akibadilishana Mawazo na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage.

No comments:

Post a Comment