Kazi ya ukarabati wa njia ya reli kati ya Tanga na
Arusha inaendelea. Mafundi wa Kampuni ya Reli Tanzania bado wapo kazini, ambapo
ukarabati wa awamu ya awali kati ya Korogwe na Mombo upo mbioni kukamilika,
bado Km 5 tu hadi kufika Stesheni ya Mombo.
Ukarabati huo wa njia ya reli ya Tanga na Arusha yenye
urefu wa Km 437 unaotarajiwa kukamilika mwaka 2018 mwezi Juni, unahusisha
uwekaji mataluma na reli katika maeneo yaliyoathirika kutokana na wizi wa
miundombinu ya reli unaofanywa na baadhi ya wananchi wasio waaminifu, pamoja na usafi wa njia hiyo ikiwemo uondoaji wa nyasi na miti iliyoota kwenye njia hiyo.
Matukio zaidi katika picha
Ukarabati wa wa njia ya reli ya Tanga na Arusha umelenga
kurudisha upya safari za treni kwa abiria na mizigo ambazo zilikuwa zimesimama
kwa muda mrefu, ufufuaji huo utahusisha pia matengenezo makubwa na madogo ya
Vituo vya treni na magenge ya wafanyakazi yaliyopo katika njia hiyo ya reli.
Sehemu ya ofisi ya kituo
cha treni cha Korogwe ikiwa tayari imefanyiwa ukarabati mdogo katika baadhi ya
sehemu ukijumuisha fenicha na majengo ya ofisi ya kituo hicho.
|
NAPONGEZA HATUA YA KUIFUFUA RELI HIYO YA TANGA ARUSHA, NAKUMBUKA MIAKA YA NYUMA NILITUMIA USAFIRI SANA WA TRENI HIYO KWENDA MOSHI, NA KUNA DEREVA WA GARI MOSHI WA NJIA HIYO ALIKUWA MAARUFU JINA LAKE ALIKUWA AKIITWA YONA, ILA NASIKIA KWA SASA NI MAREHEMU>
ReplyDelete