Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amefanya ziara mkoani Tanga kwenye mradi wa
ukarabati wa njia ya reli kati ya Tanga na Arusha yenye urefu wa KM 437, ambapo
kipande cha njia ya reli kati ya Korogwe na Mombo chenye urefu wa KM 46 tayari
umekamilika.
Katika ziara hiyo Waziri
Mbarawa ameipongeza kampuni ya reli Tanzania kwa jitihada zake za kuboresha
huduma na kuchangia pato la taifA, ambapo kwa mwaka 2015/2016 kampuni ya reli
Tanzania imefanikiwa kusafirisha Tani 100,087 za mizigo, mwaka 2016/2017
imesafirisha mizigo Tani 200,093 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 57. Kwa
upande wa abiria Kampuni imefanikiwa kusafirisha abiria kwa mwaka 2015/2016 imesafirisha abiria
483,660 2016/2017 600,030 huku treni za mjini Dar es Salaam zikiwa
zimesafirisha abiria 1,020,000 kwa mwaka 2015/2016 na mwaka 2016/2017
imesafirisha abiria 5,100,037.
Pia Waziri Mbarawa
amemuagiza Mkurugenzi wa Kampuni ya Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa
akishirikiana na watendaji wake kuongeza idadi ya mizigo na abiria
wanasafirishwa kwa njia ya reli na hivyo kuongeza pato katika kampuni hiyo.
Aidha Waziri Mbarawa
ameagiza kukamilika kwa ukarabati wa njia ya reli ya Tanga, Moshi hadi Arusha
ifikapo mwezi April mwaka 2018, na kuongeza kuwa ili kuhakikisha ufanisi wa
huduma ya usafiri kwenye njia hiyo serikali tayari imefanya mazungumzo na
wamiliki wa vichwa kumi na moja vya treni vilivyopo bandarini na tayari iko
kwenye mchakato wa kuvinunua vichwa hivyo kumi na moja.
Waziri Mbarawa amewatoa
wasiwasi wananchi kuhusu uzima na ubora wa vichwa hivyo kwa kusema kuwa,
serikali iliunda kamati maalum ya wataalam kwa ajili ya kuvifanyia uchunguzi
vichwa hivyo juu ya ubora wake na kujihakikishia kuwa vichwa hivyo ni vipya na
vina ubora stahiki.
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa na mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Reli
Tanzania Ndg. Masanja Kagodosa wakielekea kupanda trolley tayari kwa safari ya
kuelekea stesheni ya Mombo, trolley hiyo iliwawezesha kushuhudia njia ya reli iliyokarabatiwa na kusafiri kwa kupitia njia hiyo kutoka Korogwe hadi Mombo.
|
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimpa maelekezo mkurugenzi mkuu wa Kampuni
ya Reli Tanzania Ndg. Masanja Kagodosa
|
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akihutubia wakazi wa Mombo waliohudhuria
mkutano uliofanyika kwenye ziara hiyo ndogo.
|
No comments:
Post a Comment