MAFUNDI WA TRL WAMEKARABATI NJIA YA RELI INAYOELEKEA BANDARINI KATIKA ENEO LA DARAJA LA TPA BENDERA TATU - TRC Blog

Home Top Ad

"TOGETHER WE MOVE"

Monday, November 13, 2017

MAFUNDI WA TRL WAMEKARABATI NJIA YA RELI INAYOELEKEA BANDARINI KATIKA ENEO LA DARAJA LA TPA BENDERA TATU


Mvua zilizonyesha hivi karibuni zimesababisha uharibifu wa miundombinu ya reli na maji katika eneo la Daraja la TPA Bendera tatu, mafundi wa TRL na DAWASCO wamewasili eneo hilo na tayari wameanza kazi ya ukarabati wa miundombinu hiyo pamoja na uondoaji mchanga uliojaa kwenye njia ya reli kutokana na mvua hizo.  
Mkurugenzi mkuu wa Uendeshaji wa TRL Ndugu Focus Sahani(wa tatu kushoto) akiwa na Mkuu wa kitengo Biashara Nugu Shaban Kiko (wa kwanza kushoto) wakijadiliana na wataalaam wa DAWASCO.
Mkurugenzi Mkuu wa Uendeshaji Ndugu Focus Sahani(aliyevalia fulana yenye mishari) akifatilia marekebisho ya njia ya reli katoka Daraja la TPA-Bendera Tatu kufuatia mvua kubwa ziliizonyesha na kusababisha mchanga kujaa kwenye njia ya reli na kusababisha mafuriko.
 
Mafundi wa DAWASCO wakiwa kazini wakiendelea na kazi ya kukarabati miundombinu ya maji iliyoharibika kutokana na mvua

Mafundi wa TRL wakiendelea na kazi ya kuttoa mchanga uliojaa kwenye njia ya Reli.


Daraja hilo la bendera tatu linapitisha magari makubwa na mengi kutokana na shughuli nyingi za usafirishaji mizigo kutoka bandarini. Pia ndio njia ya reli ambayo hutumika kupitishia mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam. 
Mkurugenzi mkuu wa Uendeshaji wa TRL Ndugu Focus Sahani akipata maelekezo kutoka kwa maafisa wa TRL.






No comments:

Post a Comment