Ukarabati wa njia ya reli
kati ya Tanga na Arusha unaendelea kwa kasi, ambapo kwa hivi sasa mafundi
wanakarabati kipande cha reli kati ya Korogwe na Mombo. Tayari Km 27 kati ya Km
46 za kipande hicho cha njia ya reli umekamilika, huku mafundi wakiendelea na
km 19 zilizobaki hadi kufika stesheni ya Mombo.
Ukarabati wa njia hiyo ya
reli ambao ulianza tarehe 02 Oktoba 2017 unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa
mwezi Desemba mwaka 2017 kwa kipande cha Korogwe hadi Mombo.
Kukamilika kwa ukarabati huo
kunatarajiwa kusaidia shughuli nyingi za kiuchumi, kijamii pamoja kuongeza
ajira kupitia usafiri wa reli ambao ulikuwa umezorota katika njia hiyo tangu
mwaka 2008 na kuathiri shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii.
Mafundi
wakipakia mataluma na vyuma vya reli katika Stesheni ya Korogwe kwa ajili ya
kwenda kufanyia ukarabati sehemu za njia ya reli zilizoharibika kutokana na
wizi wa vyuma vya reli.
|
Mafundi
wakiwa wamebeba vyuma vya reli kuvipeleka katika sehemu inayotakiwa kufanyiwa
ukarabati.
|
Mafundi
wakiondoa kifusi kilichofunika njia ya reli katika eneo la Makuyuni
|
Mafundi
wakiendelea na kazi ya kusafisha njia ya Reli katika eneo la Makuyuni
|
Mafundi
wakifunga vyuma vya reli kwenye mataluma katika makutano ya njia ya reli na
barabara eneo la Makuyuni
|
|
Mafundi
wakifunga vyuma vya reli kwenye mataluma katika makutano ya njia ya reli na
barabara eneo la Makuyuni
|
Sehemu
ya njia ya reli katika eneo la Makuyuni ikiwa tayari imefanyiwa usafi na
kuondolewa kifusi kilichofunika reli
|
No comments:
Post a Comment