Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Ndg.
Masanja Kungu Kadogosa amefanya mkutano na wafanyakazi wa TRL na RAHCO ili
kujadili utendaji kazi wa kampuni hizo mbili na namna ya kuendelea kuboresha
utendaji kazi wa kampuni hizo mbili kwa lengo la kuongeza ufanisi katika
usafiri wa reli Tanzania.
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania Ndg. Masanja Kungu Kadogosa akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania na Kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli. |
Kadogosa alizungumzia kuhusu
mabadiliko ambayo yanatarajiwa kutokea kwenye kampuni hizo mbili, ambapo
linatarajiwa kuundwa shirika moja ambalo litakuwa linashughulika na shuhguli
zote za reli ikiwemo ujenzi, usimamiaji wa rasilimali za reli na utoaji wa
huduma za reli,na kuwataka wafanyakazi kuwa tayari na mabadiliko hayo ili
kwenda sambamba na kasi ya serikali katika ufanyaji kazi.
Pia Mkurugenzi Kadogosa
alisema kuwa mabadiliko yanayotarajiwa kutokea yatakuwa ni makubwa yatahusisha
mabadiliko ya fenicha za maofisini, magari pamoja na hali bora ya kiutendaji
“TRC tunayokwenda sio ile
iliokuwa hata ‘organization’ sio ile tuliyokuwa nayo ila itakuwa ni ya
tofauti”, “Kuna watu hawapendi haya mabadiliko, mabadiliko yanayokuja ni
makubwa ikiwemo magari sehemu zote, Dar es salaam, Morogoro, Tabora, fenicha za
maofisini pia na hali bora ya kiutendaji” alisema Ndg. Kadogosa
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania Ndg. Masanja Kungu Kadogosa akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya Reli Tanzania na Kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli
|
Pamoja na hayo Ndg.
Kadogosa amesisitiza kuwa serikali haina mpango wa kumuachisha mtu kazi
isipokuwa kwa wale watakaojitakia wenyewe, pia amesisistiza kuwa serikali
kupitia wizara itaunda kamati itakayosimamia suala zima la kuundwa kwa Shirika
jipya la Reli litakalotokana na RAHCO na TRL ambapo litaitwa Tanzania Railyways
Cooperation (TRC). Na itawekwa wazi ni kwa namna gani kampuni hizo mbili
zitaungana na namna ambavyo maslahi ya wafanyakazi yakavyowekwa, pia
amesisitiza kuwa hakuna mfanyakazi atakayepunguziwa mshahara.
Mkurugenzi mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Reli Tanzania Ndg. Masanja Kungu Kadogosa akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania na Kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli
|
Wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania na
Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu Ndg. Masanja
Kungu Kadogosa
|
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Reli
Tanzania akiuliza swali kwa Menejimenti.
|
Wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu Ndg. Masanja Kungu Kadogosa |
No comments:
Post a Comment