Kampuni ya Reli Tanzania imeanza kazi ya kurudisha huduma ya usafiri wa mizigo na abiria kati
ya Tanga na Arusha ambayo ilisitishwa kwa takribani muda wa miaka kumi tangu
mwaka 2008 kutokana na changamoto za kiutendaji, hatua hiyo ni moja kati ya
mikakati ya kampuni katika kuboresha huduma ya usafiri wa abiria na
usafirishaji mizigo nchini Tanzania.
Kipande cha reli kati ya Stesheni ya Korogwe na Maurui kikiwa tayari kimefanyiwa ukarabati.
|
Maboresho ambayo yapo mbioni
kumalizika na kuanza safari zake mara tu matengenezo ya reli yatakapokamilika
ni kutoka Dar es salaam hadi Mombo na kuanza safari zake mara moja baada ya
kukamilika.
Akizungumza kwenye mkutano
na waandishi wa habari kwenye ofisi za Kampuni ya Reli Tanzania Mkurugenzi Mkuu
Ndg. Masanja Kungu Kadogosa amesema kuwa ufufuaji wa njia hiyo ya reli utaleta
ufanisi kwenye kurahisisha shughuli za kiuchumi katika Mikoa ya Tanga na
Arusha.
Ndg. Masanja
ameongeza kuwa ukarabati huo unakwenda kwa kasi hadi kufikia mapema mwakani
safari za treni za mizigo na abiria kati ya Dar es Salaa na Tanga kwenye
stesheni ya Mombo utakuwa umeanza kufanya kazi ikiwa ni awamu ya kwanza huku
mafundi wakiendelea na ukarabati wa njia hiyo ili kutimiza lengo la kurudisha
safari za treni hadi Arusha.
Mafundi wakiweka kifusi katika tuta la reli
ambalo lilikuwa limeathirika na mmomonyoko wa udongo.
|
No comments:
Post a Comment