Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.
Mhandisi Atashasta Nditiye ambaye ni naibu waziri mpya wa Uchukuzi na
Mawasiliano baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kufanya mabadiliko madogo ya wizara, mawaziri na manaibu mawaziri.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Anditiye akizungumza na Menejimenti ya TRL pamoja na waandishi wa habari wasili katika ofisi za TRL jijini Dar es Salaam |
Naibu waziri Anditiye amefanya ziara hiyo
ikiwa ni muendelezo wa ziara zake katika taasisi za uchukuzi na mawasiliano nchini,
kwa lengo la kupata taarifa za maendeleo ya miradi mbalimbali ya taasisi zilizo
chini ya wizara ya uchukuzi na mawasiliano ikiwemo Kampuni ya Reli Tanzania.
Katika ziara hiyo Naibu waziri Mhandisi
Anditiye amepatiwa taarifa za miradi mbali mbali ya Kampuni ya Reli Tanzania
ikiwemo mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa inayotumia umeme(SGR) ambao mpaka
hivi sasa umetimu miezi sita, mradi wa ufufuaji wa reli kati ya Tanga na
Arusha, treni za abiria za mjini na zinazoenda mikoani pamoja na zile
zinazoenda mjini.
Pia Mhandisi Anditiye amepatiwa taarifa za
hatua za ziada ambazo Kampuni ya reli zinachukua kuboresha huduma za usafiri wa
reli nchini. Mkurugenzi mkuu wa uendeshaji Ndg. Focus Sahani amemueleza naibu
waziri kuwa kampuni imefanyia ukarabati wa njia za reli, mabehewa na injini.
Aidha Mkurugenzi Mkuu Ndg. Masanja Kungu
Kadogosa ameeleza mafanikio ambayo mpaka sasa kampuni ya Reli Tanzania limepata
kufuatia uboreshaji wa huduma ya usafiri wa reli Tanzania.
Naye naibu Waziri Atashasta Anditiye ameahidi ushirikiano kwa Kampuni ya Reli Tanzania katika kuhakikisha utendaji kazi unaimarika zaidi.
Naye naibu Waziri Atashasta Anditiye ameahidi ushirikiano kwa Kampuni ya Reli Tanzania katika kuhakikisha utendaji kazi unaimarika zaidi.
No comments:
Post a Comment