Mkurugenzi mkuu wa uendeshaji
wa Kampuni ya Reli Tanzania Ndg. Focus Sahani ametembelea ukarabati wa njia ya
reli kati ya Tanga na Arusha katika eneo la stesheni ya Maurui, iliyopo
Wilayani Korogwe mkaoni Tanga.
Ndg. Sahani ameridhishwa na
utendaji kazi wa mafundi ambao wanafanya ukarabati wa njia hiyo tangu mwezi
Agosti na mpaka sasa zaidi ya KM 16 zimekamilika, huku km 30 zikibaki kufanyiwa
ukarabati hadi kufika Stesheni ya Mombo. Ukarabati huu ni wa awamu ya kwanza
ambao unaanzia Stesheni ya Korogwe hadi Mombo.
Ukarabati wa njia hiyo
unahusisha usafishaji wa njia hiyo ikiwemo kuondoa vifusi vilivyokuwa
vimefunika reli, kuondoa nyasi, miti pamoja na visiki vilivyokuwa vimeota kwenye njia hiyo kutokana
na kutotumika kwa njia hiyo ya reli kwa muda mrefu.
Lengo la ukarabati wa njia
hiyo ya reli ni kurudisha safari za abiria na mizigo kutoka Stesheni ya Dar es
salaam hadi Tanga, Moshi na Arusha ambayo itasaidia katika kukuza uchumi lakini
pia kuboresha huduma ya usafiri wa reli nchini.
No comments:
Post a Comment