Kampuni ya Reli Tanzania
katika kuhakikisha linatoa huduma inayoendana sambamba na kasi ya serikali ya
awamu ya tano, imeamua kufufua kichwa cha treni aina ya SUK 2927 ambacho
kilikuwa kinatumia makaa ya mawe kama nishati ya kuendeshea chombo hiko.
Kichwa hiko kilichokuwa
miongoni mwa vichwa arobaini vya aina hiyo vilivyokuwa vikifanya shughuli ya
usafirishaji wa mizigo na abiria nchini Tanzania na Afirca Mashariki kuanzia
mwaka 1954, kinafanyiwa matengenezo ili kirudi kati shughuli hiyo ya
usafirishaji mizigo na abiria ili kuongeza kasi ya ufanisi ya utoaji huduma,
lakini pia kichwa hiko cha treni kinaweza kuwa sehemu ya Utalii kutokana na Historia
iliyoibeba.
Kichwa hiko kwa hivi sasa
hakitumii tena nishati ya makaa ya mawe, bali kinatumia nishati ya mafuta ya
dizeli ambapo mfumo wa matumizi ya makaa ya mawe ulibadilishwa mwaka 1998 na kuanza kutumia nishati ya mafuta ya
dizeli.
No comments:
Post a Comment