Tanzania
na Rwanda zimekubaliana kujenga reli ya kisasa(SGR) yenye urefu wa km400 kutoka
Isaka-kigali, mradi ambao utasaidia usafirishaji wa bidhaa na kukuza biashara
baina ya nchi hizo mbili.
Makubaliano
hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe. Paul Kagame
yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam kufuatia ziara ya kikazi ya siku moja
ya Rais Paul Kagame.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Rwanda
Paul Kagame
|
Rais
Magufuli amesema kuwa wamewaelekeza mawaziri wa miundombinu wa nchi hizo mbili
kukutana wiki inayofuata kujadili namna ya kuwezesha mradi huo kifedha.
Mazungumzo hayo ya mawaziri hao wawili yatazingatia namna ya ufadhili wa mradi
huo kabla ya kutangazwa tenda, Magufuli amesema kuwa jiwe la msingi litawekwa
mwisho mwa mwaka huu 2018.
Reli
hiyo inatarajiwa kuunganisha Dar es Salaam na Kigali kupitia Isaka na kuboresha
usafirishaji wa bidhaa kutoka ndani na nje ya Rwanda, kwa kuzingatia kwamba
takribani asilimia 60 ya mizigo inayotoka na kuingia Rwanda inapitia bandari ya
Dar es Salaam.
Mtandao
wa reli ya kisasa(SGR) unatarajiwa kuunganisha nchi za Afrika Mashariki,
Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda ambapo tayari Kenya imejenga reli
hiyo ya Kisasa inayounganisha jiji la Mombasa na Nairobi, huku Tanzania na
Uganda zikiwa tayari ziemeanza mchakato wa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa.
Tanzania
inajenga reli ya kisasa (SGR) kwa awamu mbili kutoka Dar es Salaam hadi
Morogoro ambayo itakuwa na urefu wa km330 na Morogoro hadi Makutupora (Dodoma)
ambayo itakuwa na urefu km426 zikitumia fedha za ndani takribani dola za
kimarekani Bilioni 3.
Ni jambo jema kuona viongozi wetu wana mtazamo wa mbele wa secta hii ua usafirishaji hasa kuhusiana na suala zima la kupunguza gharama na pia kuweza kusafirisha mizingo mingi na mizito ambayo ingepita katika barabara zetu ingesababisha uharibifu wa barabara hizo.
ReplyDeleteNa pongeza uamuzi huo walioufikia!
Uncle Magufuli Songa mbele usiangalie wala kugeuka myuma.....wala usisimame wewe kazamwendo tuu.....mpaka kieleweke , big up sana kwako Rais wetu kipenzi.....
ReplyDelete