Wakati Ujenzi wa Reli ya kisasa Ukishika kasi kutoka Dar Es
Salam hadi Morogoro yenye urefu wa kilomita 300 baadhi ya wakazi wasio
waaminifu wametajwa kuhusika na wizi wa mafuta kwa kushirikiana na baadhi ya
madereva wanaofanya kazi kwenye mradi huo.
Jeshi la Polisi kikosi maalumu cha Reli Nchini kwa kushirikiana
na maofisa kadhaa wa Shirika la reli Tanzania(TRC) wamefanikiwa kuyakamata
madumu yenye lita 2510 za mafuta aina ya disel na madumu matupu 94
yaliyoibwa kutoka kambi ya Ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa (Standard Gauge)
ya Ngerengere ambako Ujenzi wa mradi huo unafanyika.
Sehemu ya madumu 94 ya mafuta yaliyokamatwa katika kambi ya Ngerengere yakiwa na Lita 2510 za mafuta ya
Dizeli pamoja na baadhi ya vifaa walivyokuwa wakivitumia.
|
Sehemu ya madumu 94 ya mafuta yaliyokamatwa katika kambi ya Ngerengere yakiwa na Lita 2510 za mafuta ya
Dizeli. Waliopiga magoti ni watuhumiwa waliokamatwa na madumu hayo ya mafuta.
|
Sehemu ya madumu ya mafuta 94 yaliyokamatwa katika kambi ya Ngerengere
yakiwa na Lita 2510 za mafuta ya Dizeli. Kutoka kulia ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania Catherine Mushi akiwa na Mkuu wa Polisi kikosi cha Reli Kamanda Salum Kisai.
Katika tukio hilo watuhumiwa wanne wanashikiliwa na Jeshi la
Polisi katika kituo cha polisi cha Ngerengere Mkoani Morogoro Kwa uchunguzi
zaidi na kisha watafikishwa Mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.
No comments:
Post a Comment