Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa leo hii ametangaza rasmi kuanza kutumika kwa Sheria
mpya ya shirika la Reli TRC Act na. 10 Ya 2017.
Katika tukio hilo lililofanyika
mbele ya Katibu Mkuu wa wizara hyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika
la Reli Prof.John Kondoro. Waziri amesema wafanyakazi waliokuwa RAHCO na
TRL watahamia katika shirika la Reli na kuwa mali na madeni yote ya RAHCO na
TRL yatahamishiwa kwenye Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Katika hatua nyingine mhe. Waziri
alimtangaza Bw Masanja Kadogosa kuwa ameteuliwa NA Rais Wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi mpya wa shirika la reli na
Prof Kondoro John atakuwa ndio Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Shirika hilo.
Ujumbe huo pia ulitembelea maeneo ya
shauri moyo na kuona kazi ya ya ujenzi wa nguzo za njia ya reli mpya ambayo
kuanzia hapo itapita juu mpaka kuingia stesheni ya Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa akikabidhi Sheria
mpya ya reli kwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania
Prof. John Kondoro
|
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa akikabidhi Sheria
mpya ya reli kwa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Ndg. Masanja Kadogosa
|
Serikali kupitia Bunge la
jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 13 septemba 2017 lilipitisha kuanzishwa
kwa sheria ya Reli ya Tanzania. Aidha, tarehe 8 Oktoba 2017, Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt John Pombe Magufuli
aliridhia sheria tajwa, na tarehe 13 Oktoba 2017 sheria ya Reli Tanzania
ilitangazwa kwenye gazeti la serikali.
Lengo kuu la Sheria ya Reli
Tanzania ni kutoa huduma bora ya usafiri kwa njia ya reli, utunzaji na uendeshaji
wa miundombinu ya Reli.
Matokeo ya kutungwa kwa sheria
ya Reli ni pamoja na kufuta sheria ya Reli Na.4 ya mwaka 2002 na kufutwa kwa iliyokuwa kampuni
Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) na kampuni ya Reli Tanzania(TRL).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akitazama eneo ambalo kazi ya ujenzi wa daraja la Km 2.9 litakalopita reli ikianza.
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame
Mbarawa (wa tano kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa msimamizi wa mradi wa SGR Eng. Maizo Mgedzi.
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame
Mbarawa (wa pili kushoto) akiwahamasisha wananchi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha mradi unakwenda kwa wakati.
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame
Mbarawa akiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya watumishi wa TRC na Yapi Merkezi.
|
No comments:
Post a Comment