Rais Dk.John Magufuli leo ameweka jiwe la
Msingi la Ujenzi wa awamu ya pili ya Reli ya Treni ya Umeme kutoka
Morogoro-Dodoma-Makutupora katika eneo la Ihumwa, Manispaa ya Dodoma kwa
kumtaka Mkandarasi Yapi Merzeki kutoka Uturuki kukamilisha ujenzi wa Reli hii
ndani ya muda ili Watanzania waanze kuona manufaa ya Reli hii ambayo itasaidia
katika kukuza Uchumi wa Nchi na kurahisisha sekta ya Usafirishaji nchini
Tanzania.
Reli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 10,000 ambazo ni sawa na malori 500 yenye tani 20 kila moja ukilinganisha na reli ya zamani(metre gauge) ambayo hata ikifanyiwa maboresho haiwezi kufikia kiwango hiko, reli hiyo itasaidia kukuza uchumi wa nchi, kupunguza uharibifu wa mazingira, kusafirisha abira na mizigo na abiria kwa unafuu, uharaka na usalama lakini pia itaokoa barabara zetu kutokana na uharibifu unaotokana na mizigo mikubwa inayobebwa na malori.
Rais Magufuli ameongeza kuwa Reli hii yenye gharama ya zaidi ya Tsh Trilioni 4 inajengwa kwa fedha za walipa kodi bila kupata ufadhili wowote na hivyo kutoa rai kwa Watanzania kulipa Kodi ili itumike kwa ajili ya kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali. Wakati huo huo Rais Magufuli ameahidi ujenzi wa barabara ya lami kutoka barabara kuu ya Dar es salaam kuingia ndani eneo la Ihumwa.

Akimkaribisha Rais, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa amemuhakikishia Mh Rais kwamba atasimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi CCM ili kuwaletea Watanzania maendeleo katika nyanja mbalimbali na kuwataka Watanzania kuchangamkia fursa zitakazotokana na ujenzi wa Reli hii ya Kati.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa na Mkurugenzi wa TRC Ndg Massanja Kadogosa,kwa nyakati tofauti,wameelezea mradi huu wa Reli kama kati ya miradi michache inayotekelezwa Afrika na hivyo kuiweka Tanzania katika nchi zilizopiga hatua kubwa katika sekta ya Usafirishaji.
Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amempongeza Mh Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya maendeleo ambayo yanaigusa Dodoma kwa kiwango kikubwa na kuwataka wanaDodoma wachangamkie fursa za ujenzi wa Reli na maendeleo makubwa yanayotokana na Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.

Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo
la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma
yenye urefu wa km 426 ukijumuisha na njia za kupishana katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
|
Treni
ya zamani ikipita katika Reli za zamani katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani
Dodoma.
|
Mtendaji
Mkuu wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa akitoa maelezo ya mradi huo wa
Reli ya kisasa ya umeme kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli
|
Sehemu
ya wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi.
|
Muonekano
wa moja ya vituo vya treni vitakavyojengwa kwenye mradi huo wa SGR kutoka Morogoro hadi Makutupora
|
Muonekano
wa moja ya mahandaki ya njia za treni yatakayojengwa kwenye mradi wa awamu ya pili ya SGR kutoka Morogoro hadi Dar es Salaam
|
Muonekano
wa daraja la juu la treni ya umeme
|
No comments:
Post a Comment