Historia ya reli nchini
Tanzania inatajwa kuanza kuwapo visiwani Zanzibar miaka ya 1880 chini ya
utawala wa Sultani Bargash ambaye alijenga reli visiwani humo yenye urefu wa Km
10 ikiunganisha Hekalu lake lililokuwa Chukwani kisiwani humo na maeneo ya
mjini.
Reli ya Tanganyika ilianza kujengwa na utawala wa Wajerumani kuanzia Tanga mwaka 1893 na kufika Muheza mwaka 1896, Mombo 1905 na Moshi 1911. Utawala huo ulianzisha kampuni iliyoitwa ‘Germany Colonial Railway Construction and Administration Company’ kwa lengo la kuiendesha reli ya Tanga-Moshi (‘the Usambara Railway’) amabayo ilianza kufanya kazi mwaka 1912. Uamuzi wa kuiendeleza reli hadi Arusha ulifikiwa mwaka 1911 na ujenzi ulikamilika 1929 na reli kufunguliwa mwaka huo huo na Gavana wa wakati huo ‘Sir Donald Cameron’.
Kituo cha treni cha Tanga mwaka 1890. Katika kituo hiki ndiko reli ilikoanza kujengwa mwaka 183.
|
Upimaji wa Reli ya Kati
(‘Central line’) kuunganisha DSM na ziwa Tanganyika ulifanywa mwaka 1894 na
ujenzi kuanza mwaka 1905; ikafika Tabora 1912 na Kigoma mwaka 1914.
Mtandao wa Reli kabla na baada ya uhuru wa Tanganyika.
|
Kituo cha Treni cha Mikese
mkoani Morogoro mwaka 1909.
|
Kituo cha Treni cha Tabora mwaka 1910.
|
Kituo cha Treni cha Morogoro mwaka 1912.
|
Kituo cha Treni cha Kidete
mkoani Morogoro mwaka 1914.
|
Ujenzi wa reli chini ya
wakoloni uliendelea hadi mwaka 1960 ambapo reli ya Kilosa kwenda Mikumi
ilijengwa. Reli nyingine zilizojengwa kipindi cha ukiloni wa Mwingereza na ile
ya kiunganishi cha Kenya na Tanzania, yaan kutoka Voi hadi Kahe mnamo mwaka
1924. Hali kadhalika, mwaka 1932 reli kutoka Manyoni hadi Singida ilijengwa na
mnamo 1933 ikafika Kinyangiri eneo lililokuwa mashuhuri kwa uzalishaji wa
karanga. Hata hivyo, iling’olewa na baadaye kujengwa upya na Serikali ya
Tanzania kuanzia Manyoni mwaka 1985 na kufika Singida mwaka 1997.
Ujenzi wa reli kutoka
Msagali hadi Kongwa ulianza mnamo mwaka 1947 na baada ya miaka miwili yaan 1949
reli hiyo ilifika Hogoro (Kongwa) eneo lililokuwa mashuhuri kwa uzalishaji wa
karanga. Hata hivyo, reli hii iling’olewa baadaye. Mwaka 1949 hadi 1958 reli ya
Nachingwea-Ruo-Chilungula na Masasi mkoani Mtwara ilijengwa, japo ilikuja
kung’olewa mwaka 1963.
Mwaka wa 1963, reli kutoka
Mruazi hadi Ruvu Junction ilijengwa na serikali ya Tanganyika ili kuunganisha
reli ya Tanga na ya reli ya Kati. Huo ndiyo mtiririko wa ujenzi wa reli kuanzia
wakoloni hadi baada ya uhuru.
MADHUMUNI
YA WAKOLONI KUJENGA RELI
Lengo kuu la Wajerumani
kujenga reli lilikuwa kusafirisha mazao ya biashara kama katani, kahawa, pamba,
karanga, ngano, mpira n.k. kutoka maeneo ya uzalishaji kwenda kwenye masoko
ndani na nje ya nchi, ili kukidhi mahitaji yaliyotokana na mapinduzi ya viwanda
(Industrial revolution). Sambamba na hilo walianzisha usafirishaji wa abiria.
Baadhi ya Injini zilizokues
zikitumika wakati wa Ukoloni kusafirisha abiria na mizigo.
|
MUUNDO
YA RELI BAADA YA UHURU
Baada ya Tanganyika kupata
Uhuru tarehe 9 Desemba, 1961; Serikali mpya iliendelea kutoa huduma ya
kusafirisha abiria na mizigo kwa msukumo zaidi. Nchi tatu za Afrika Mashariki
Kenya, Uganda na Tanzania ziliungana na kuunda Jumuiya ya Afrika Mashariki
(‘East Africa Community’) mwaka 1967 kwa lengo la kuunganisha nguvu katika
nyanja za usafirishaji na mawasiliano.
Shirika la Reli na Bandari
la Afrika Mashariki (‘East Africa Railways and Harbours’) ni kati ya taasisi
zilizoundwa kuwezesha biashara na mawasiliano kati ya nchi hizi tatu na watu
wake. Wananchi wa nchi hizi wakawa huru kutembeleana na kufanya biashara kwa
kutumia barabara, reli, meli na ndege. Usafiri wa ndege ulikuwa chini ya
Shirika la Ndege na mawasiliano yalifanyika kupitia Shirika la Posta la Afrika
Mashariki.
Shughuli za Ishara na
mawasiliano ya Reli kwa wakati huo zilisimamiwa na kitengo maalum cha Shirika
la Posta na Simu la Afrika Mashariki (‘East African Posts and
Telecommunication- EAP&T’).
Shirika la Reli na Bandari
Afrika Mashariki lilitenganishwa na kuundwa taasisi mbili zinazojitegemea za
Shirika la Reli Afrika Mashariki (‘East Africa Railways Corporation’) na
Shirika la Bandari Afrika Mashariki (‘East Africa Harbours Corporation’).
Shirika la Reli Afrika Mashariki lilianzishwa rasmi tarehe 1 juni, 1969 ambapo
madhumuni yake makuu yalikuwa na usafirishaji wa mizigo na abiria kwa nchi
wanachamna na nchi jirani (landlocked).
Ili kupata kiunganishi
kizuri cha usafiri wa abiria na mizigo kwa nchi jirani, Shirika la Reli
lilitumia usafiri wa majini (meli) kupitia maziwa ya Victoria, Nyasa na
Tanganyika. Baadhi ya meli zilizotumika ni Mv. Victoria. Ziwa Tanganyika
lilikuwa na meli za Mv. Liemba, Mwongozo na Sangara. Ziwa Nyasa lilikuwa na
meli za Mv.Iringa na Mv Songea.
Usafririshaji wa mizigo na
abiria uliendelea kuwa kazi madhubuti ya Shirika la Reli Afrika Mashariki
ambalo lilikuwa na uwezo wa kubeba mizigo mikubwa na mingi kwa wakati mmoja.
Mazao yaliyosafirishwa kipind cha Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliendelea kuwa
yale ya kipindi cha ukoloni, pamoja na kwamba uliongezeka usafirishaji wa
bidhaa za viwandani. Jumuia ya Afrika Mashariki ilileta ufanisi mzuri wa
usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka nchi moja hadi nyingine.
Kituo cha Treni cha Dar es
Salaam mwaka 1972
|