TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJALI ILIYOTOKEA MKOANI KIGOMA - TRC Blog

Home Top Ad

"TOGETHER WE MOVE"

Wednesday, June 6, 2018

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJALI ILIYOTOKEA MKOANI KIGOMA
SHIRIKA LA RELI TANZANIA-TRC
YAH: AJALI YA BASI LA  ABIRIA KUGONGA TRENI  YA MIZIGO
KATIKA ENEO LA GUNGU MKOANI  KIGOMA
Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania-TRC unapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu ajali ya basi la abiria kugonga treni ya mizigo na kusababisha vifo vya watu kumi, kati yao wanawake watatu na wanaume saba na majeruhi thelathini na mbili.
Ajali imetokea jana tarehe 6 Juni, 2018 majira ya saa 12:15 Asubuhi katika eneo la Gungu  Mkoani Kigoma. Ajali hiyo imesabababishwa na basi la kampuni ya Princess Hamida lenye namba za usajili T885DLD, aina ya TATA, lililokuwa likiendeshwa na Fredy Kawasange  kutoka Kigoma kwenda Tabora. Basi hilo limegonga treni ya mizigo yenye injini namba 88U15 iliyokuwa ikitoka  Kazuramimba  kwenda Kigoma.
Chanzo cha ajali kimetokana na uzembe wa dereva kutofuata sheria za barabarani. Dereva huyo wa  basi hakusimama  mita 15 kabla ya  kivuko chetu  cha gari Moshi na hivyo kusababisha ajali hiyo.
Miili ya marehemu imehifadhiwa  katika Hospitali ya Mkoa, Kigoma - Maweni kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi, na majeruhi wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo ya Maweni.
Shirika la Reli Tanzania-TRC linawapa pole wanafamilia wote walioguswa na ajali hiyo na kusababisha majeruhi na vifo vya ndugu, jamaa na marafiki. Shirika linazidi kuwaombea wawe na moyo wa subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu. Shirika linaungana na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awapumzishe Marehemu mahala pema peponi na Majeruhi wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kila siku.
Imetolewa na;
Idara ya Uhusiano kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Reli Tanzania
Dar es Salaam.
07/06/2018.No comments:

Post a Comment