KAIMU MKURUGENZI WA TRC ATEMBELEA KILOSA KUONA MAENDELEO YA UIMARISHAJI WA NJIA YA RELI KATI YA KILOSA NA GULWE - TRC Blog

Home Top Ad

"TOGETHER WE MOVE"

Friday, May 4, 2018

KAIMU MKURUGENZI WA TRC ATEMBELEA KILOSA KUONA MAENDELEO YA UIMARISHAJI WA NJIA YA RELI KATI YA KILOSA NA GULWE


\Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania Ndg. Focus Sahani Makoye amefanya ziara kwenye eneo la Kilosa kukagua maendeleo ya uimarishaji wa njia ya reli kati ya Kilosa na Gulwe, sehemu ambayo iliathiriwa zaidi na mafuriko yaliyosababishwa na mvua mwishoni mwa mwaka jana na kusababisha safari za treni kutoka Dar es Salaam kuelekea Bara kusitishwa kwa muda kwa takribani miezi miwili.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Ndg. Focus Sahani(wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya wahandisi na Afisa Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania Mohamed Mapondela(wa kwanza kushoto) walipowasili site Kilosa.
Katika hatua nyingine Serikali imesema ifikapo mwezi wa saba mwaka huu wananchi wote wanaoendesha shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo kandokando ya reli waache mara moja pindi watakapovuna mazao yao ili kulinda reli kutokana na ukweli kwamba shughuli za kibinadamu zinazoendelea kandokando ya reli zimechangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa mafuriko katika eneo hilo la Kilosa hadi Gulwe.
Tamko hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Ndg. Atashasta Nditiye ambaye pia amefanya ziara katika eneo hilo kwa nyakati tofauti kwa lengo la kujionea maendeleo ya ukarabati wa tuta la reli ambalo liliathiriwa Vibaya na Mafuriko mwishoni mwa mwaka jana.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Fokasi Sahani amewapongeza wafanyakazi wa Shirika hilo pamoja na wahandisi waliofanikisha kurejea kwa safari za Treni, huku akizungumzia zoezi la upandaji wa matete kandokando ya tuta la reli ambayo yatasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Ndg. Focus Sahani akiwa na baadhi ya maofisa kutoka Shirika la Reli Tanzania wakikagua Karavati, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha mafuriko hayafiki kwenye tuta la reli. 


Moja kati ya makaravati mapya ambayo yamejengwa kwenye tuta la reli kati ya Kilosa na Gulwe ili kuruhusu maji kupita kwenye njia sahihi bila kuleta athari kwenye tuta la reli..


Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Ndg. Focus Sahani(wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya wahandisi na Afisa Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania Mohamed Mapondela(wa kwanza kushoto) wakikgua maendeleo ya uimarishaji wa tuta la reli kati ya Kilosa na Gulwe.


No comments:

Post a Comment