WEZI WA MAFUTA KAMBI YA RELI YA KISASA (SGR) YA NGERENGERE WAKAMATWA. - TRC Blog

Home Top Ad

"TOGETHER WE MOVE"

Wednesday, April 4, 2018

WEZI WA MAFUTA KAMBI YA RELI YA KISASA (SGR) YA NGERENGERE WAKAMATWA.


Wakati Ujenzi wa Reli ya kisasa Ukishika kasi kutoka Dar Es Salam hadi Morogoro yenye urefu wa kilomita 300 baadhi ya wakazi wasio waaminifu wametajwa kuhusika na wizi wa mafuta kwa kushirikiana na baadhi ya madereva wanaofanya kazi kwenye mradi huo. 

Jeshi la Polisi kikosi maalumu cha Reli Nchini kwa kushirikiana na maofisa kadhaa wa Shirika la reli Tanzania(TRC) wamefanikiwa kuyakamata madumu  yenye lita 2510 za mafuta aina ya disel na madumu matupu 94 yaliyoibwa kutoka kambi ya Ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) ya Ngerengere ambako Ujenzi wa mradi huo unafanyika. 

Sehemu ya madumu 94 ya mafuta yaliyokamatwa katika kambi ya Ngerengere yakiwa na Lita 2510 za mafuta ya Dizeli pamoja na baadhi ya vifaa walivyokuwa wakivitumia. 
Sehemu ya madumu 94 ya mafuta yaliyokamatwa katika kambi ya Ngerengere yakiwa na Lita 2510 za mafuta ya Dizeli. Waliopiga magoti ni watuhumiwa waliokamatwa na madumu hayo ya mafuta.
Sehemu ya madumu ya mafuta 94 yaliyokamatwa katika kambi ya Ngerengere yakiwa na Lita 2510 za mafuta ya Dizeli. Kutoka kulia ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania Catherine Mushi akiwa na Mkuu wa Polisi kikosi cha Reli Kamanda Salum Kisai.

Tukio hili la kukamatwa Kwa madumu haya ya mafuta lilifanywa na kikosi Maalum cha Jeshi la Polisi kitengo cha Reli, kazi ya ukamataji wa mafuta hayo ilifanywa mnamo tarehe 3 mwezi wa nne mwaka 2018 saa nne na dakika 22 usiku hadi tarehe 4 mwezi wa 4 mwaka 2018 saa 2 na dakika 20 asubuhi ndipo walipofanikiwa kuwatia watuhumiwa hao nguvuni wakiwa na madumu hayo ya mafuta aina ya Diseli.

Katika tukio hilo watuhumiwa wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha polisi cha Ngerengere Mkoani Morogoro Kwa uchunguzi zaidi na kisha watafikishwa  Mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.

             

No comments:

Post a Comment