WAZIRI MBARAWA ATANGAZA RASMI SHIRIKA LA RELI TANZANIA-TRC - TRC Blog

Home Top Ad

"TOGETHER WE MOVE"

Saturday, March 3, 2018

WAZIRI MBARAWA ATANGAZA RASMI SHIRIKA LA RELI TANZANIA-TRC

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa leo hii ametangaza rasmi kuanza kutumika kwa Sheria mpya ya shirika la Reli  TRC Act na. 10  Ya 2017.  
Katika tukio hilo lililofanyika mbele ya Katibu Mkuu wa wizara hyo na Mwenyekiti wa Bodi  ya Shirika la  Reli Prof.John Kondoro. Waziri amesema wafanyakazi waliokuwa RAHCO na TRL watahamia katika shirika la Reli na kuwa mali na madeni yote ya RAHCO na TRL yatahamishiwa kwenye Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Katika hatua nyingine mhe. Waziri alimtangaza Bw Masanja Kadogosa kuwa ameteuliwa NA Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi mpya wa shirika la reli na Prof Kondoro John atakuwa ndio Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Shirika hilo.
Ujumbe huo pia ulitembelea maeneo ya shauri moyo na kuona kazi ya ya ujenzi wa nguzo za njia ya reli mpya ambayo kuanzia hapo itapita juu mpaka kuingia stesheni ya Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa akikabidhi Sheria mpya ya reli kwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania Prof. John Kondoro
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa akikabidhi Sheria mpya ya reli kwa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Ndg. Masanja Kadogosa
Serikali kupitia Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 13 septemba 2017 lilipitisha kuanzishwa kwa sheria ya Reli ya Tanzania. Aidha, tarehe 8 Oktoba 2017, Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt John Pombe Magufuli aliridhia sheria tajwa, na tarehe 13 Oktoba 2017 sheria ya Reli Tanzania ilitangazwa kwenye gazeti la serikali.     
Lengo kuu la Sheria ya Reli Tanzania ni kutoa huduma bora ya usafiri kwa njia ya reli, utunzaji na uendeshaji wa miundombinu ya Reli.
Matokeo ya kutungwa kwa sheria ya Reli ni pamoja na kufuta sheria ya Reli Na.4  ya mwaka 2002 na kufutwa kwa iliyokuwa kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) na kampuni ya Reli Tanzania(TRL).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wataalamu kutoka Yapi Merkez kuhusu jinsi madaraja yatakavyojengwa kuanzia kituo cha Dar es Salaam hadi Ilala alipotembelea kambi ya Ilala.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa  (wa pili kushoto) akitazama eneo ambalo kazi ya ujenzi wa daraja la Km 2.9 litakalopita reli ikianza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa  (aliyeketi) akiendesha mtambo wa kuchimba mashimo maalum ya nguzo za madaraja kuashiria kuanza kwa ujenzi wa daraja kutoka kituo cha Dar es Salaam hadi Ilala.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa (wa tano kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa msimamizi wa mradi wa SGR Eng. Maizo Mgedzi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa  (wa pili kushoto) akiwahamasisha wananchi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha mradi unakwenda kwa wakati.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa  akiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya watumishi wa TRC na Yapi Merkezi.





No comments:

Post a Comment