HUDUMA YA USAFIRI WA TRENI KUTOKA DODOMA KUELEKEA TABORA, MWANZA, KIGOMA NA MPANDA KUENDELEA KAMA KAWAIDA - TRC Blog

Home Top Ad

"TOGETHER WE MOVE"

Monday, January 15, 2018

HUDUMA YA USAFIRI WA TRENI KUTOKA DODOMA KUELEKEA TABORA, MWANZA, KIGOMA NA MPANDA KUENDELEA KAMA KAWAIDA


Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) unawataarifu abiria wote na wananchi kwa Ujumla  kuwa kutokana na kuharibiwa kwa miundombinu ya reli kati ya  stesheni za Kilosa na Gulwe kurokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha maeneo hayo  huduma za reli kutoka Dar es Salaam zimesitishwa.
Hata hivyo Uongozi baada ya kutathmini hali ya miundombinu ya maeneo mengine yalio salama imeamua kuhamishia huduma ya usafiri wa treni kutokea Dodoma kuanzia siku ya Jumanne Januari 16, 2018.
Ratiba ya huduma ya muda kuanzia Dodoma ni kama  ifuatavyo..         


Uongozi wa TRL bado unaendelea kusimamia kazi ya ukarabati wa eneo lililo haribika kati ya Kilosa na Gulwe. Aidha Kampuni inaomba radhi Kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi ambacho huduma ya usafiri wa treni haitakuwepo mpaka hapo itakaporejeshwa tena, wananchi watafahamishwa rasmi kupitia vyombo vya habari.


Sehemu ya Reli ikiwa imeharibiwa vibaya na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha mafuriko kwenye njia ya reli.

            

No comments:

Post a Comment