WAZIRI PROF. MAKAME MBARAWA AMEFANYA ZIARA MKOANI TANGA KWENYE MRADI WA UKARABATI WA NJIA YA RELI KATI YA TANGA NA ARUSHA - TRC Blog

Home Top Ad

"TOGETHER WE MOVE"

Saturday, December 16, 2017

WAZIRI PROF. MAKAME MBARAWA AMEFANYA ZIARA MKOANI TANGA KWENYE MRADI WA UKARABATI WA NJIA YA RELI KATI YA TANGA NA ARUSHA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amefanya ziara mkoani Tanga kwenye mradi wa ukarabati wa njia ya reli kati ya Tanga na Arusha yenye urefu wa KM 437, ambapo kipande cha njia ya reli kati ya Korogwe na Mombo chenye urefu wa KM 46 tayari umekamilika.
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisikiliza maelezo kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania Ndg. Masanja Kagodosa mara baada ya kuwasili stesheni ya Korogwe

Katika ziara hiyo Waziri Mbarawa ameipongeza kampuni ya reli Tanzania kwa jitihada zake za kuboresha huduma na kuchangia pato la taifA, ambapo kwa mwaka 2015/2016 kampuni ya reli Tanzania imefanikiwa kusafirisha Tani 100,087 za mizigo, mwaka 2016/2017 imesafirisha mizigo Tani 200,093 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 57. Kwa upande wa abiria Kampuni imefanikiwa kusafirisha abiria  kwa mwaka 2015/2016 imesafirisha abiria 483,660 2016/2017 600,030 huku treni za mjini Dar es Salaam zikiwa zimesafirisha abiria 1,020,000 kwa mwaka 2015/2016 na mwaka 2016/2017 imesafirisha abiria 5,100,037.         
Pia Waziri Mbarawa amemuagiza Mkurugenzi wa Kampuni ya Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa akishirikiana na watendaji wake kuongeza idadi ya mizigo na abiria wanasafirishwa kwa njia ya reli na hivyo kuongeza pato katika kampuni hiyo.
Aidha Waziri Mbarawa ameagiza kukamilika kwa ukarabati wa njia ya reli ya Tanga, Moshi hadi Arusha ifikapo mwezi April mwaka 2018, na kuongeza kuwa ili kuhakikisha ufanisi wa huduma ya usafiri kwenye njia hiyo serikali tayari imefanya mazungumzo na wamiliki wa vichwa kumi na moja vya treni vilivyopo bandarini na tayari iko kwenye mchakato wa kuvinunua vichwa hivyo kumi na moja.
Waziri Mbarawa amewatoa wasiwasi wananchi kuhusu uzima na ubora wa vichwa hivyo kwa kusema kuwa, serikali iliunda kamati maalum ya wataalam kwa ajili ya kuvifanyia uchunguzi vichwa hivyo juu ya ubora wake na kujihakikishia kuwa vichwa hivyo ni vipya na vina ubora stahiki.  
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa na mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania Ndg. Masanja Kagodosa wakielekea kupanda trolley tayari kwa safari ya kuelekea stesheni ya Mombo, trolley hiyo iliwawezesha kushuhudia njia ya reli iliyokarabatiwa na kusafiri kwa kupitia njia hiyo kutoka Korogwe hadi Mombo.






Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na baadhi ya vijana walioshiriki kwenye kazi ya ukarabati wa njia ya reli ya Tanga na Arusha, kipande cha Korogwe hadi Mombo mara baada ya kuwasili stesheni ya Mombo.
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimpa maelekezo mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania Ndg. Masanja Kagodosa


Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akihutubia wakazi wa Mombo waliohudhuria mkutano uliofanyika kwenye ziara hiyo ndogo.

Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania Ndg. Masanja Kagodosa akihutubia wakazi wa Mombo waliohudhuria mkutano uliofanyika kwenye ziara hiyo ndogo.

Sehemu ya wakazi wa Mombo wakisiliza hotuba kutoka kwa Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.




No comments:

Post a Comment